Back to top

Wananchi Bonde la Kilombero wapanda hekta 1300 za miti.

11 July 2018
Share

Zaidi ya hekta elfu moja na mia tatu za miti ya kupandwa aina ya Mitiki zimepandwa na wananchi wa vijiji 43 vya wilaya za Kilombero, Malinyi na Ulanga mkoani Morogoro miti ambayo mbao zake zina thamani kubwa kuliko mbao nyingine zozote za miti ya kupandwa Duniani.

Wakiongea na ITV baadhi ya wananchi walioanza kupanda miti hiyo mwaka 2015 wamesema kwa sasa wameanza kunufaika na ufadhili wa kuendeleza mashamba yao kutoka kitengo cha wakulima wa nje wa kampuni ya Mitiki bonde la Kilombero KVTC ambayo inatoa huduma mbalimbali za ugani kuendeleza mashamba yao mpango ambao umeongeza hamasa kwa wananchi wengi kujihusisha na upandaji wa miti aina ya Mitiki.

Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya taasisi ya utafiti wa misitu Tanzania TAFORI Dkt.Felician Kilahama ambae amewatembelea wakulima hao katika vijiji vya Mbingu, Ngajengwa, Njage na Mngeta wilayani Kilombero amesema kilimo hicho cha miti ni muhimu kwani kinaendana na sera ya serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ya viwanda kupitia sekta ya misitu ambapo meneja wa wakulima wa nje wa kampuni ya mitiki ya bonde la Kilombero KVTC, Bw.Keneth Kayuni amesema mpango huo unazingatia hifadhi ya mazingira isiyoathiri vyanzo vya maji na misitu ya asili.