
Naibu Waziri wa Ardhi Mhe.Geophrey Pinda, amewataka wananchi wa Kisaki katika Manispaa ya Singida mkoa wa Singida, kuhakikisha wanadumisha amani muda wote wa kushughulikia migogoro ya ardhi kwenye maeneo yao.
Naibu Waziri Pindaamebainisha hayo wakati wa kutafuta suluhu ya mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa Kisaki na Mwekezaji wa Sekta ya Nyuki katika eneo la Kisaki B Manispaa ya Singida mkoani Singida.
Naibu Waziri Pinda amefika Kijiji cha Kisaki kilichopo mpakani mwa Manispaa ya Singida na Wilaya ya Ikungi mkoani Singida lengo likiwa kusikiliza na kutatua mgogoro wa ardhi baina ya Wananchi na Mwekezaji wa Nyuki.
Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Kisaki Moses Shaban amesema, maneno yaliyozungumzwa na Naibu Waziri Mhe Geophrey Pinda kuhusu utatuzi wa mgogoro baina ya wananchi na Mwekezaji ni tunu yenye afya na mbolea katika kutatua mgogoro wa ardhi katika eneo hilo.
"Umeongoza kikao kilaini na kitamu hata aliyekuwa na hasira zimepotea na hata yule aliyekuwa na silaha ameshusha nakupongeza sana". Aliongeza Diwani Shaban
Mhe.Pinda mewata wananchi wa Kijiji cha Kisaki kwenda kuanza vikao vya suluhu ya mgogoro wao na suala la kukutana na serikali basi Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Singida italisimamia kwa kuwa suala hilo lishatoka katika ngazi ya Kijiji.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili ameeleza kuwa Mgogoro wa ardhi baina ya wananchi wa Kijiji cha Kisaki na Mwekezaji wa Sekta ya Nyuki, katika eneo la Kisaki B ulifika ofisini kwake mwaka 2022 ambapo wananchi walidai maeneo kutwaliwa Mwekezaji.
Hata hivyo, mkuu huyo wa Wilaya ya Singida amesema, kufuatia kadhia hiyo aliunda Tume ili kubaini kama madai ni ya kweli au la ambapo Tume ilimalia kazi mei 2023 na kupeleka mrejesho katika ofisi yake oktoba 2023.
