Back to top

Wananchi Kaliua Tabora wakumbwa na hofu ya upungufu wa chakula.

14 January 2020
Share

Baadhi ya wananchi wilayani Kaliua mkoani Tabora wameanza kuwa na hofu ya kuwepo kwa upungufu wa chakula baada ya mazao yanayotegemewa kwa chakula kudumaa kutokana na kiwango cha mvua kuongezeka  hivyo wameiomba serikali kuwahimiza watafiti na wazalishaji wa mbegu za mazao ya chakula kutafuta mbegu zinazokabiliana na hali ya mvua nyingi.

Wamesema kuendelea kunyesha kwa mvua nyingi katika wilaya hiyo kumekuwa kukiwasababishia hofu na kuomba serikali kuona haja ya kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuwasaidia kuepuka kukumbwa na njaa licha ya kuwa mvua nyingi haiwezi kuzuilika.

Akitoa takwimu za hali ya chakula ya upatikanaji wa chakula afisa kilimo,umwagiliaji na ushirika wa wilaya ya Kaliua Eveline Ngwira amesema wananchi wa vijiji kumi wako hatarini kukosa chakula cha kutosha katika msimu uliopita na kwamba ipo haja ya kuweka akiba ya chakula kitakachopatikana ili kukabiliana na hali hiyo.