Back to top

Wananchi Karatu watengeneza barabara ya Km.40 kufuata huduma za jamii

19 July 2020
Share

Mamia ya wafugaji  wa jamii ya Watatoga wakazi wa kijiji cha Endesh tarafa ya Eyasi wilayani Karatu wamekusanyika kufyeka msitu mnene wakitengeneza barabara ya zaidi ya kilometa arobaini kwenda hospitali ya Hydom na chanzo cha mto Endesh hili kupunguza kero za kutembea umbali mrefu kufuata huduma za kijamii


ITV ilifika kwenye kijiji hicho na kushuhudia wafugaji hao wakiwa na zana za asili Mapanga, Shoka,Sululu,Majembe na zingine wakifyeka huku wakiwaomba wadau wa maendeleo wawaunge mkono.