Back to top

Wananchi kata ya Mlimani Morogoro wadhamiria kuwapiga mawe watalii.

17 April 2021
Share

Wananchi wa mitaa ya Chalagule, Choma na Mbete kata ya Mlimani manispaa ya Morogoro wamedai kuwa watawapiga mawe watalii wa kigeni na wa ndani wanaofanya utalii kwenye kivutio cha utalii cha maporomoko marefu ya maji kwa madai kuwa wanajisaidia kwenye mashamba na bustani zao kutokana na eneo hilo kutokuwa na vyoo kwa ajili ya watalii hao.
.
Wananchi hao wameyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na wananchi wenyewe kwa ajili ya kutafuta suluhisho la changamoto zinazoikabili mitaa yao.
.
Kufuatia hali hiyo ITV imeutafuta uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ambapo Afisa Habari wa Manispaa hiyo Bi.Lilian Heneriko amesema kuwa watafika eneo hilo ikiwezekana watajenga choo cha dharura kwenye eneo hilo ili kuondoa kero kwa wananchi.