Back to top

Wananchi kata ya Mwandiga wilayani Kigoma walalamika kukosa maji

06 December 2019
Share

Wananchi wa kata ya Mwandiga katika halmashauri ya wilaya ya Kigoma wamelalamikia kata hiyo yenye zaidi ya watu elfu kumi kukosa huduma ya maji licha ya kuwepo mradi wa maji ambao ulishindwa kutoa maji kwa miaka mingi.

Wamemweleza waziri wa maji Mh. Profesa Makame Mbarawa kuwa kata hiyo ilikuwa na mradi wa maji wa Mkongoro lakini haukuweza kusaidia kutatua tatizo la maji na kutaka mradi mpya unaendelea kukamilika kwa wakati ili kuondoa adha wanayopata wananchi

Kwa upande wake mhandisi wa maji wa mamlaka ya maji safi na taka mjini Kigoma Jones Mbike amesema mradi huo utakuwa suluhisho la tatizo la maji katika kata ya Mwandiga huku waziri wa maji Mhe. Profesa Makame Mbarawa akieleza kuwa mradi huo unaotokana na mradi mkubwa wa maji Kigoma Ujiji utakamilika katika kipindi cha miezi miwili ijayo na ukitumia zaidi ya shilingi milioni mia tisa