Back to top

Wananchi Kigoma walaani ukatili kwa wanawake na watoto.

07 December 2018
Share

Baadhi ya wananchi  wa kata ya Msambara wilayani Kasulu mkoani Kigoma wamelaani vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vinavyofanywa na baadhi ya wanaume  na kisha  kutokomea kusikojulikana huku wakiziacha familia zao zikiteseka jambo kwa kuwa tegemezi katika jamii.
 
  
Wakizungumza wakati wa kilele cha siku 16 za kupinga vitendo vya Ukatili wa kijinsia wamesema vitendo hivyo vimekuwa vikiongezeka kila kukicha ambapo wameiomba serikali na wadau wa mbalimbali kusaidia kutoa elimu ili kusaidia kupunguza hali hiyo.
 
 
Mratibu wa masuala ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na wasichana kutoka shirika la umoja wa mataifa la UN Women Lucy Tesha amesema mkoa wa Kigoma ni miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa kuwa na kiwango kikubwa cha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na kwamba mpango wa pamoja Kigoma utasaidia kuondoa changamoto hiyo.