Back to top

Wananchi Kigoma waomba serikali kuingilia kati ubambikizwaji wa ankara

10 May 2021
Share

Baadhi ya wananchi katika manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma wamelalamikia  tabia ya baadhi ya maafisa wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Kigoma KUWASA kuwababimbikizia zaidi ya kiwango cha malipo ya ankara ya matumizi ya maji huku wengine wakiwa hawapati huduma na kuiomba serikali kudhibiti hali hiyo ambayo imekuwa ikiwatatiza kwa muda mrefu sasa.


Wananchi hao wamesema wamekuwa wakipewa kiwango kikubwa cha matumizi ya maji tofauti na walivyotumia maji huku wengine wakilazimika kulipia elfu ishirini kila mwezi bila kupata huduma ya maji.


Akitoa ufafanuzi kaimu Mkurugenzi wa KUWASA Josephat Rwegasila amesema kuwepo kwa changamoto hiyo, ikiwa ni siku moja baada ya mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji nchini EWURA kuitaja KUWASA kuwa kinara  sugu wa kuwabambikizia wateja kiwango kikubwa cha ankara za maji,kaimu mkurugenzi wa kuwasa josephat rwegasila amesema.