Wananchi wa vijiji vinne vilivyopo kata ya Sedeko wilaya Serengeti mkoani Mara wameiomba serikali pamoja na wadau kuwasaidia kuwajengea bweni ili kuwalinda watoto wao wasishambuliwe na wanyama wakati wa kwenda shule na kurejea nyumbani.
ITV imefika katika vijiji hivyo ambavyo ni Bisarasara Bonchuku ,Sedeko na Nyamburi ambavyo viko mpakani mwa Hifadhi ya Serengeti na kushuhudia wananchi hao wakiwa wamejenga madarasa nane, maabara mbili na majengo mawili ya utawala kwa garama ya zaidi ya shilingi milioni mia mbili kwa nguvu zao.
Wananchi hao wameungana kwa pamoja na kuchangishana fedha kupitia makundi rika na wadau mbalimbali na kujenga shule mbili ndani ya kata moja ambazo ni Sedeko na Nyamburi.