
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema hadi kufikia Julai 18, 2022 jumla ya wananchi Mil. 11.5 nchini sawa na 37% wamepata chanjo kamili ya Uviko-19.
.
Waziri Ummy ameyasema hayo alipokutana na viongozi wa dini mkoani Tanga na kufanya nao kikao kilicholenga kutoa elimu na hamasa ya Chanjo ya Uviko-19 ambapo amewataka viongozi hao kuwa mabalozi wa chanjo hiyo kwa waumini wao.
