Back to top

Wananchi tumieni fursa ya uwepo wa Kituo cha Uwezeshaji.

01 April 2022
Share

Bodi ya Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi imewashauri wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kutumia fursa ya uwepo wa Kituo cha Uwezeshaji kiuchumi kilichopo Kahama kujiongezea uwezo na ujuzi wa kufanya uwekezaji wenye tija.


 
Kauli hiyo imetolewa na Makamu Mwenyeki wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi. Anna Maembe wakati akiongoza bodi hiyo kukagua kituo hicho cha uwezeshaji wananchi  kiuchumi cha Kahama.

Nao baadhi ya wadau wanaounda kituo hicho ambacho ni jumuishi ikiwemo Taasisi ya Serikali ya GS 1 inayotoa alama za utambuzi wa bidhaa kimataifa (Msimbo Milia) imesema  kuwa kituo hicho kimekuwa chachu ya maendeleo ya jamii hasa kwa wajasiriamali wadogo na wa kati.