Back to top

Wananchi wa Malolo wilayani Kilosa wamejitolea kujengea kituo cha afya

18 September 2019
Share

Wananchi wa kata ya Malolo wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro wamejitolea kujenga kituo cha afya baada ya adha ya kusafiri umbali wa kilometa zaidi ya 40 kwaajili ya kufuata huduma za  matibabu katika wilaya za jirani ikiwemo wilaya ya Kilolo mkoani Iringa huku waziri mkuu Kassim Majaliwa akitoa onyo kali kwa watumishi wa vituo vya afya na zahanati kote nchini kuacha kuwauzia wagonjwa dawa kinyume na taratibu.

Ameyasema hayo katika uwekaji wa jiwe la msingi  katika kituo cha afya cha kata ya Malolo wilayani Kilosa ulioambatana na harambee kwaajili ya ujenzi wa kituo hicho iliyowezesha kupatikana kwa shilingi milioni 20 huku waziri mkuu akiwa amechangia shilingi milioni tano ambapo  wananchi wakawa na haya ya kusema.

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali itaendelea kuunga mkono jitihada za wananchi na kwamba mtumishi yeyote atakayeshindwa kutoa huduma nzuri kwa wananchi serikali haitamfumbia macho.

Aidha waziri mkuu pia amefanya mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Mikumi ambapo amewataka watanzania kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali.