Back to top

Wananchi wa Ukonga wapewa Barakoa kujikinga na Corona

21 May 2020
Share

Shirika lisililo la kiserikali la Neema Edward Mkwelele Wellness Foundation, limegawa barakoa kwa Serikali za Mitaa ya Ukonga Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu COVID-19.

Shirika la Neema Foundation limejikita katika kusaidia jamii ya kitanzania hasa kwa watoto, mabinti, vijana na akina mama kufikia hali bora kielimu na kiuchumi ili kutatua changamoto zinazopelekea umasikini katika jamii.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini humo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikali hilo, Expedita Nyoni, amesema kuwa wametoa barakoa hizo kutokana na wao kuamini kwamba kuna baadhi ya watu katika jamii ambao hawana uwezo wa kumudu kununua barakoa na ni kitu ambacho ni hatari zaidi na kinaweza kuwasababishia kupata maambukizi ya ugonjwa huo, hivyo wameamua kugawa barakoa hizo bure ili kulinda afya za wengi

Nyoni amesema Uongozi wa Shirika la Neema Foundation, unatoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Tanzania kwa juhudi inazozichukua katika kupambana na ugonjwa huo kwa kushirikia na wadau kutoka katika taasisi mbalimbali.