Back to top

Wananchi waaswa kuacha kuchoma ovyo misitu mkoani Ruvuma

01 December 2019
Share

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bi. Christina Mndeme amewataka wananchi kuacha  tabia ya kuchoma hovyo misitu ili kufanikisha mradi mkubwa wa upandaji miti katika hekta  elfu hamsini eneo la Ifinga halmashuri ya wilaya ya Madaba.
 
Bi.Mndeme amesema kuwa mradi huo unaotekelezwa na wakala wa  huduma za misitu Tanzania(TFS) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali unakwenda kuupaisha mkoa wa Ruvuma kiuchumi na hivyo changamoto ya uchomaji moto misitu inapaswa kushughulikiwa.
 
Afisa misitu wa mkoa wa Ruvuma Bw.Africanus Challe anasema mradi huo unakwenda kuchochea uwekezaji mkubwa kwenye viwanda vya mbao na bidhaa zitokanazo na miti,
 
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri  ya wilaya ya Madaba Bw.Shafii Mpenda anasema mradi huo umetoa ajira na unatarajiwa kutoa ajira zaidi kwa wananchi ambapo milioni mia nane zinatumika kwa mwaka kwa ajili kusafisha mashamba ya miti katika mradi huo.