Back to top

Wananchi wachangishana fedha kujenga zahanati Kahama.

12 November 2019
Share

Wananchi wa kijiji cha Itumbo kata ya Kisuke wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameilalamikia serikali ya halmashauri ya Ushetu kutokamilisha ujenzi wa zahanati ambayo wameijenga kwa nguvu zao wakiwa na lengo la kuzuia vifo vya wanawake wajawazito na watoto wachanga wanaojifungulia njiani wakitembea kufuata huduma kwa zaidi ya kilomita 12 katika vijiji vya jirani.

Licha ya malalamiko hayo wananchi wa kijiji cha Itumbo wamesema wamechoka kuisubiri serikali na kumuita mbunge wao ili ashuhudie wakichangishana wenyewe fedha za kukamilisha ujenzi wa zahanati hiyo.

Naye mkurugenzi wa wa halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama Bw.Michael Matomota akizungumzia changamoto ya kutembea umbali mrefu ni mtambuka kulingana na vijiji vingi kukosa zahanati lakini kituo cha afya cha halmashauri kinatarajiwa kukamilika siku za karibuni na kuanza kutoa huduma ambapo kitapunguza changamoto ya wagonjwa kutembea umbali mrefu kwa baadhi ya maeneo.

Kwa upande wake naibu waziri wa ujenzi Mhe.Elias Kwandikwa ambaye pia ni mbunge wa jimbo hilo amesema serikali ya awamu ya tano inaendelea kutoa fedha za ujenzi wa majengo ya zahanati na vituo vya afya katika vijiji,kata na wilaya lengo likiwa ni kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi na kutatua changamoto mtambuka ya wagonjwa kutembea umbali mrefu.