Back to top

Wananchi wafunguka kilichosababisha ugumu kusajili laini za simu.

21 January 2020
Share

Wananchi mkoani Arusha walioshindwa kusajili namba zao za simu wamesema kukosekana kwa mfumo mzuri vitendeakazi na wataalam wa  kutosha katika zoezi hilo ni miongoni mwa sababu zilizochangia usumbufu na wameiomba serikali kujenga utamaduni wa kuwa na   maandalizi ya kutosha kunapokuwa na majukumu ya msingi yanayoihusu jamii.

Wananchi hao wameyasema hayo wakati wa siku ya mwisho ya kujiandikisha ambapo licha ya kukiri kuwepo kwa baadhi ya changamoto kwa  upande wao wamesema zilizoko nupande wa serikali ni kubwa zaidi.

Afisa msajili wa mamlaka ya vitaambulisho vya taifa mkoa wa Arusha Bi. Julieth Raimond na mkuu wa wilaya ya Arusha Bw.Gabriel Dakharo  wanaelezea changamoto hiyo na hatua zinazochukuliwa.

Pamoja na changaamoto hizo hadi ofisi za NIDA zinafungwa asilimia kubwa ya wananchi walikuwa wameshapata huduma.