Back to top

WANANCHI WAFURAHISHWA NA MSAADA WA KISHERIA DAR

09 July 2024
Share

Wananchi walionufaika na huduma ya msaada wa Kisheria inayotolewa na Serikali kupitia Kampeni ya Mama Samia legal Aid, wamesema wamefurahishwa na huduma hiyo na kuwataka wananchi wengine kuchangamkia fursa hiyo inapofika kwenye maeneo yao, kwani huduma hiyo imewapa mwanga wa namna ya utatuzi wa matatizo yao kisheria bila gharama. 

Mkurugenzi msaidizi wa Sheria Wilaya ya Temeke, Elias Mkapa na Mkurugenzi wa Mbagala Paralegal Bi.Joyce Ephraim, wametoa wito kwa Wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kupata msaada wa Kisheria unaotolewa bure hadi tarehe 13 Julai 2024, kwenye banda la Wizara ya katiba na Sheria lilipo kwenye viwanja vya maonesho ya Sababa Temeke - Dar- es Saalam.

Bi.Eluminata Alphonce Mkazi wa Tabata Bima, ambaye ameeleza kudhulumiwa haki yake Mkoani Kilimanjaro amesema amezunguka sana kutafuta haki yake bila mafanikio lakini baada ya kusikia kuwa Rais wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan Vanatoa msaada wa kisheria bure kupitia Mama Samia Legal Aid Campaign (#MSLAC) ndipo alipofika hapo akiwa na Mawazo mengi lakini mpaka anaondoka yale Mawazo yamepungua baada ya kupata Wanasheria waliompa moyo kwamba haki yake anaweza kuipata muda na saa yoyote.