Back to top

Wananchi waiomba serikali kusaidia ujenzi wa zahanati Mbinga.

21 July 2019
Share

Wananchi wa kijiji cha mitambotambo katika halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, wameiomba serikali kusaidia kukamilisha ujenzi wa zahanati yao ambayo wameijenga kwa nguvu zao na kukwama vifaa vya kiwandani ili waweze kuondokana na adha kubwa wanayopata kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya hospitali ya misheni ya Litembo wilayani humo.
 
Wananchi hao wa kijiji cha Mitambotambo kilichopo katika wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma ambacho kina wakazi zaidi ya 800, wamesema pamoja kujitolea kujenga zahanati hiyo kwa nguvu zao, wamekwama vifaa vya kiwandani hivyo wanaiomba serikali kuwasaidia kuikamilisha ili waweze kuepukana na adha za wagonjwa wao kufariki wakiwa njiani kwenda hospitali ya misheni ya Litembo kufuata huduma za afya.
 
Hata hivyo mbunge wa jimbo la Mbinga vijijini, mheshimiwa Martin Msuha aliyetembelea zahanati hiyo ameagiza uongozi wa kijiji hicho kuandaa bajeti ya mahitaji yote yanayohitajika na kuahidi kusaidia kuikamilisha kwa manufaa ya wananchi.