Back to top

Wananchi walalamikia Upatikanaji dawa kituo cha afya Nguruka.

26 March 2018
Share

Upatiakanji hafifu wa dawa na vifaa tiba katika kituo cha afya Nguruka wilayani Uvinza mkoani Kigoma , umelalamikiwa na wananchi ambao wamekuwa wakikosa baadhi ya dawa na kulazimika kwenda kunua nje ya kituo licha ya serikali kuongeza maradufu bajeti ya ununuzi wa dawa nchini.

Kutokana na hali hiyo wameiomba serikali kubadili mfumo wa utoaji dawa na kufanya ufuatiliaji katika zahanati, vituo vya afya na hospitali ili kujiridhisha na matumizi yake pamoja na kushughulikia changamoto za upungufu wa watumishi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya afya katika kituo cha afya Nguruka Rajab Seleman amesema pamoja na kamati kuwa na jukumu la kutengeneza bajeti ya mahitaji ya kituo lakini fedha zinazoletwa hazitoshelezi mahitaji huku akieleza kuwa tatizo la dawa lipo kutokana na aina ya magonjwa ambapo mganga mfawidhi katika kituo hicho DkT. Staford Chamgeni amesema utaratibu wa kuletewa fedha moja kwa moja umesaidia kupunguza tatizo la dawa kwa kiasi kikubwa katika kituo hicho ambacho kinahudumia kata tano.