Back to top

Wananchi wanaoishi jirani na kambi za jeshi kulipwa fidia - MWINYI.

19 April 2018
Share

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dakta. HUSSEIN MWINYI amesema katika mwaka ujao wa fedha ,  wizara yake imetenga fedha kwa ajili ya kufanya tathmini na kulipa fidia kwa wananchi wanaostahili, hasa wanaoishi katika maeneo jirani na kambi za jeshi.

Dakta. HUSSEIN MWINYI amesema kambi ya 41 KJ iliyoko Majimaji ili pimwa mwaka 2005 na kwamba wakati wa upimaji wananchi zaidi ya 61 walikuwepo katika eneo hilo.

Amesema katika kambi ya 843 KJ JKT iliyoko Nachingwea, halmashauri ilianisha mipaka ya kambi na kijiji cha Mkukwe na kwamba wananchi tisa ndio waliokuwa katika eneo hilo.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa amesema wizara inatambua kuwepo kwa migogoro katika maeneo mablimbali kati ya kambi za jeshi na vijiji jirani au maeneo yaliyotawaliwa na jeshi kwa maslahi mapana ya taifa.

Ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Mbunge wa Nachingwea, Mheshimiwa HASSAN MASALA aliyetaka kujua kauli ya serikali kuhusu kushughulikia migogoro ya mipaka kati ya vijiji na kambi za jeshi.