Back to top

Wananchi wanaoishi Mabondeni watakiwa kuhama - MAJALIWA

19 April 2018
Share

Waziri Mkuu, Mheshimiwa KASSIM MAJALIWA amewataka wananchi wa naoishi maeneo ya mabonde ni kuhama katika maeneo hayo ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza hasa katika kipindi hiki ambacho mvua kubwa zimeendelea kunyesha nchini ikiwemo Jijini Dar es Salaam.

Amesema licha ya juhudi kubwa za serikali kuwataka wananchi hao waondoke, wapo baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakiingiza siasa katika suala hilo na kufanya wananchi hao kushindwa kutoka katika maeneo hayo kwa kupata utetezi kutoka kwa wanasiasa.

Waziri Mkuu MAJALIWA a mesema serikali inaandaa fedha ili kuhakikisha miundombinu ya mabondeni inaboreshwa ili maji yapite vizuri na kuwataka wote wanaoishi mabonde ni waondoke ili wasipate madhara.

Waziri Mkuu amezungumza hayo wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo Mjini Dodoma ambapo pia amezungumzia mipango mbalimabli ya serikali katika kuimarisha uchumi wa nchi.