Back to top

Wananchi zaidi ya Milioni 18 kupata matibabu hospitali mpya Chato.

11 January 2021
Share

Rais wa Msumbiji, Mhe.Filipe Nyusi ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuboresha miundombinu ya afya kila mkoa.

Pia amemuomba Rais Dkt.John Pombe Magufuli kuhakikisha hospitali mpya ya Rufaa Chato inakamilika kwa wakati ili wananchi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa pamoja na nchi jirani waanze kupata matibabu ya kibingwa.

Amesema hayo alipoweka jiwe la msingi pamoja na kupanda mti katika hosipitali hiyo.

Kwa upande wake Rais Dkt.John Pombe Magufuli amesema kukamilika kwa hosipitali hiyo kutawezesha wananchi zaidi ya Milioni Kumi na Nane kupata matibabu na ameitaka Wizara ya Afya kuhakikisha ujenzi wa awamu zilizosalia zinajengwa kwa pamoja.

Waziri wa Afya Dkt.Doroth Gwajima amesema ujenzi wa hosipitali hiyo kwa awamu ya kwanza umefikia asilimia tisini na umegharimu Shilingi Bilioni kumi na nne.