Serikali mkoani Mara imesema bado inaendelea na uchunguzi wa kuwasaka watu saba wanaodaiwa kufukiwa na kifusi ndani ya mgodi wa North Mara Nyamongo na kudai wakipatikana watakamatwa kwani ni wahalifu kama walivyo wahalifu wengine.
.
Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima ameyasema hayo kufuatia tetesi juu ya watu saba wanaodaiwa kuingia ndani ya mgodi wa North Mara kwa madai yakwenda kuiba dhahabu.