Back to top

WANAODAIWA KUWA WACHAWI WAFARIKI KWA MITISHAMBA

15 March 2024
Share

Watu zaidi ya 50 wanaodaiwa kuwa ni wachawi wamefariki dunia, nchini Angola, katika kipindi cha miezi miwili, baada ya kulazimishwa kunywa mchanganyiko wa mitishamba ili kubaini kama wanafanya vitendo hivyo.
.
Imeelezwa kuwa mchakato wa kuthibitisha endapo mtu anafanya vitendo vya uchawi nchini humo, huhusisha watuhumiwa kunyweshwa, kinywaji chenye mchanganyiko wa mitishamba maarufu kama 'Mbulungo' ambapo kwa mujibu wa jamii nchini humo huamini kuwa mtu akifa baada ya kunywa kinywaji hicho, basi alikuwa akijihusisha na uchawi.
.
Polisi nchini humo wamewaonya wale wote wanaofanya hivyo, baada ya vifo vilivyotokana na imani hiyo kuongezeka kwa kasi. #RFISwahili