Back to top

WANAOFURAHIA KIFO CHA RAIS WA IRAN KUCHUKULIWA HATUA

21 May 2024
Share

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Iran, Mohammad Kazem Movahhed Azad, ameagiza watu wote wanaomtukana kwenye mitandao ya kijamii, aliyekuwa Rais wa nchi nchi hiyo Ebrahim Raisi aliyefariki katika ajali ya helikopta, wachukuliwe hatua kali.
.
Azad ametoa wito huo baada ya baadhi ya watu kuanza kuchapisha jumbe kupitia mitandao ya kijamii wakieleza furaha yao juu ya kifo cha Rais Ebrahim Raisi huku wengine wakisisitiza kuwa alihusika katika mauaji ya maelfu ya wafungwa wa kisiasa, miaka ya 1980 pamoja na kukandamiza kwa nguvu maandamano ya kuipinga Serikali. #via #BBC