
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa, aliyechaguliwa kwa mara nyingine kuiongoza nchi hiyo, amewataka wanaohoji matokeo ya uchaguzi ya wiki iliyopita wapeleke malalamiko hayo Mahakamani.
Mnangagwa ametoa Matamshi hayo baada ya kiongozi wa upinzani kusema uchaguzi huo uligubikwa na udanganyifu mkubwa.
Tume ya taifa ya uchaguzi ya Zimbabwe, ilimtangaza Rais Mnangagwa, kushinda kwa asilimia 52.6 ya kura dhidi ya mpinzani wake wa chama cha Citizens Coalition for Change, Nelson Chamisa aliyepata asilimia 44.
Chama cha Mnangagwa cha ZANU-PF kinaendelea kuongoza tangu Zimbabwe, ilipopata uhuru mwaka 1980, chini ya marais wawili ambao ni hayati Robert Mugabe na Emmerson Mnangagwa.
