Back to top

WANAOKIUKA MAADILI WACHUKULIWE HATUA - JAJI MKUU

21 June 2023
Share

Jaji Mkuu wa Tanzania na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama, Prof. Ibrahim Juma, ameziagiza kamati za maadili nchini, kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi wa mahakama wanaokiuka maadili ya kazi, ili kutoa fundisho kwa watumishi wengine wa mahakama.
.
Jaji Mkuu ameyasema hayo kwenye kikao kazi, kilichowakutanisha wadau wa Mahakama na Tume ya Utumishi wa Mahakama, kilichofanyika mkoani Kigoma, kilicholenga kuboresha huduma za mahakama.