
Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameitaka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kushirikiana na Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri kudhibiti na kutokomeza vitendo vya uvuvi haramu.
Rais Samia amebainisha hayo wakati akihutubia wananchi katika uwanja wa Nyamagana mara baada ya kuzindua na kukabidhi boti za uvuvi na vizimba vya kufugia samaki kwa wavuvi wa kanda ya ziwa.
Rais Samia ameitaka Wizara hiyo kuwachukulia hatua kali za kisheria wavuvi wanaokiuka taratibu za uvuvi salama.
Rais Samia pia amesema serikali inafanya jitihada kuinua sekta ya uvuvi nchini kwa kuimarisha utendaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili iendane na dhamira ya mageuzi yaliyokusudiwa.
