Back to top

Wanaotaka kukwamisha zoezi la chanjo ya kuzuia saratani waonywa.

20 April 2018
Share

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Bwana.DEODATUS KINAWILO ametoa onyo kwa wananchi wenye nia ya kuhujumu zoezi la chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 14 mkoani humo.

Zoezi hilo linatarajiwa kuzinduliwa Mkoani Kagera tarehe 23 mwezi huu.

Mkuu huyo wa wilaya akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja- Jenerali Mstaafu SALUM MSTAPHA KIJUU baada ya kufungua semina ya kuwajengea uwezo watakaoratibu zoezi hilo, amesema chanjo hiyo haina madhara kwa binadamu hivyo mtu yoyote ambaye ataeneza taarifa za upotoshaji atachukuliwa hatua kali za  sheria.

Akizungumza katika hafla hiyo, Dakta. THOMAS RUTACHUNZIBWA amesema lengo la mkoa huo ni kutoa chanjo kwa wasichana zaidi ya Elfu- 35.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Mhandisi RICHARD RUYANGO akizungumza kwa niaba ya wakuu wa wilaya katika mkoa huo amesema wakuu hao watasimamia zoezi hilo kwa ukamilifu na watahakikisha wasichana wote wanaolengwa wanapata chanjo hiyo.