
Waziri wa Ardhi, Dkt. Angeline Mabula ametoa onyo kwa wananchi wanaotumia hisani ya Rais Samia Suluhu Hassan kuvamia maeneo ya hifadhi yaliyomegwa na kurejeshwa kwa wananchi kutokana na kuwa na migogoro ya matumizi ya ardhi.
.
Hata hivyo, Dkt.Mabula alibainisha kuwa kinachohitajika kwa maeneo yote yaliyomegwa kwa ajili ya shughuli za wananchi ni kuandaliwa mpango wa matumizi mazuri na jukumu la mikoa ni kuhakikisha mipango ya matumizi bora ya ardhi inaandaliwa kwa maeneo yote yaliyomegwa.
