Back to top

Wanaowacheleweshea wananchi kuwaunganishia umeme kuchukuliwa Hatua.

07 May 2021
Share

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO, Dkt.Alexander Kyaruzi, ameagiza wananchi wote waliolipia huduma ya kuunganishiwa umeme kwenye nyumba zao waingiziwe haraka kwa mujibu wa taratibu na kwamba bodi hiyo haitasita kuwachukulia hatua watakaohusika kuwacheleweshea kwa makusudi wananchi  huduma hiyo.

Dkt.Alexander Kyaruzi ametoa agizo hilo mjini Songea mkoani Ruvuma mara baada ya Mwakilishi wa Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Bw.Pololet Kamando Mgema kuwasilisha kwenye bodi ya wakurugenzi wa TANESCO kuhusu kilio cha wananchi wengi kulipia huduma ya kuunganishiwa umeme kwenye nyumba zao lakini wanakaa muda mrefu bila kupata huduma hiyo.

Hata hivyo bodi hiyo imetembelea kuona mifumo ya umeme inavyofanya kazi, vifaa na ufanisi wake katika kituo cha kupoozea umeme wa gridi ya taifa ya Makambako katika eneo la Madaba na hatimaye Unangwa wilaya ya Songea.