Back to top

"WANAOWAPA UJAUZITO WATOTO WAKIKE WASAKWE"-MAJALIWA

24 November 2023
Share

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dkt.Francis Michael na Wakuu wa Wilaya zote za mkoa huo, wahakikishe wanawasaka watu wote wanaotuhumiwa kuwapa ujauzito watoto wa kike.

Waziri Mkuu amesema tangu Januari hadi sasa, mkoa huo una kesi 59 za wasichana walioacha shule kwa sababu ya ujauzito, lakini ni kesi mbili tu zimepelekwa Mahakamani na kuhoji hizo nyingine 57 ziko wapi au zimeishia wapi.

Amemwagiza Mkuu wa Mkoa na wakuu wa wilaya wakae na Kamati zao  za Ulinzi na wabainishe wahusika na wahakikishe, hatua kali zinachukuliwa dhidi ya wote waliohusika.

Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Songwe kwa ziara ya siku tatu, amesema taarifa za mkoa huo siyo kwani kesi hizo 59 ni kwa shule za sekondari na hazijumuishi shule za msingi.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewapongeza wana-Ileje kwa kujenga maabara ya kompyuta kwenye shule hiyo yenye mikondo ya Kidato cha Kwanza hadi cha Nne ili kuhimiza matumizi ya  Teknolojia ya Habari na Mawasiliano .