Back to top

Wanasheria wa serikali wapigwa marufuku kufanya kazi binafsi za uwakil

06 February 2019
Share

Mkuu wa mashtaka mkoa wa Mbeya, Ladaslaus Komanya amesema serikali imepiga marufuku wanasheria wake na wale wa taasisi za umma nchini kufanya kazi binafsi za uwakili mahakamani bila kuwa na kibali cha mwajili wao.

Amesema katika muundo mpya wa Ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, utaratibu wa wanasheria wa serikali na wale wa taasisi za umma kufanya kazi binafsi za uwakili umefutwa na hivyo akaiomba mahakama kuwabaini wanasheria watakaoendelea na utaratibu huo wa kusimamia kesi mahakamani.

Akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya sheria nchini, Jaji Mfawidhi wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Mbeya, Mhe. Robert Makaramba amesema ipo changamoto ya ukosefu wa elimu kwa wananchi wengi juu ya taratibu za kufungua kesi mahakamani na kuziendesha hali ambayo inasababisha wengi wao kukosa haki.