Back to top

WANASHERIA WAKEMEE VITENDO VYA RUSHWA KIVITENDO

29 June 2022
Share


Waziri Mkuu Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mhe.Mizengo Pinda amewataka Wanasheria wa nchi za Afrika kuwa mstari wa mbele kukemea vitendo  vya rushwa na kuonyesha kwa vitendo kwa kuikataa ili kusaidia wananchi na nchi zao kwa ujumla.

Mhe.Pinda amesema hayo Jijini Arusha wakati anafngua mkutano wa Chama Cha Wanasheria Afrika ambao pamoja na mambo mengine utajadili  athari za Arusha katika nchi za Umoja wa Afrika.

Rais wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Dr.Edward Hosea amesema Watazungumzia athari za rushwa kweye Uchumi, Haki za Binadamu, na Utawala wa Sheria.
 
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt.Peter Mathuki na Rais wa Chama Cha Wanasheria Afrika, Bw.Emaka Jude  wamesema nchi za Umoja wa Afrika Zinaweza kuondokana na changamoto zilizopo ikiwemo ya kuendelea kuwa tegemezi kama kila sekta  ikiwemo ya sheria na pia ya habari itaweza kutimiza wajibu wake kwa uhuru bila kuingiliwa na mamlaka za dola.