
Jeshi la Polisi mkoani Rukwa linawashikilia wanawake wawili, wakazi wa Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa kwa tuhuma za kuwauwa waume zao kwa kuwakata na jembe na shoka katika sehemu za kichawani kutokana na wivu wa kimapenzi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani mkoani humo, ACP Shadrack Masija amethibitisha, nakusema tukio la kwanza limetoa katika Kijiji cha Kisumba Manispaa ya Sumbawanga ambapo Priska Tenganamba (32) alimua mumewe mwenye miaka (33) kwa kumkata na Jembe sehemu za kichwani huku katika Kijiji cha Kisumba Anastazia Alex (47) akimuua mumewe mwenye miaka (55), kwa kumkata na shoka kichwani.
