
Sheikh wa Wilaya ya Sumbawanga, iliyopo mkoani Rukwa, Thabit Khamis, amewashauri wanawake mkoani humo kuisaidia serikali kupinga na kukemea vitendo vya ushoga dhidi ya watoto pamoja na kuwalea katika mazingira bora na misingi ya dini ili kuwaepusha na vitendo viovu ikiwemo ulawiti na ubakaji.
.
Sheikh Thabit ameyasema hayo kwenye sherehe ya Jumuia ya Wanawake wa Kiisilamu zilizofanyika katika msikiti wa Majengo uliopo Manispaa ya Sumbawanga, mkoani humo.