Back to top

Wanjala auawa na wananchi. - Kenya.

15 October 2021
Share

Masten Wanjala mtuhumiwa aliyekiri kuwaua zaidi ya watoto kumi na baadaye kutoroka katika kituo cha polisi alipokuwa anazuiliwa ameuawa na wanakijiji wa Bungoma Magharibi mwa Kenya. 

Naibu Kamishna wa Kaunti ya Bungoma Cornelius Nyaribai amethibitisha kifo chake katika ujumbe wa Twittter.

Polisi wanasema Masten Wanjala alifuatwa na wanakijiji hadi nyumbani katika mji wa Bungoma na kupigwa hadi kufa.

Mamlaka ilikuwa imeanzisha msako mkali kumtafuta mtu huyo ambaye alikiri kuwaua zaidi ya wavulana kumi katika kipindi cha miaka mitano.

Masten Wanjala alitoweka kutoka kwa selo za polisi katika mji mkuu, Nairobi .

Maafisa watatu wa polisi wa Kenya waliokuwa kazini siku walifikishwa mahakamani siku ya Alhamisi na kufunguliwa mashtaka ya kumsaidia mtuhumiwa huyo.

Bwana Wanjala alikamatwa mnamo Julai na alikiri kutumia dawa za kulevya na kuwaua wavulana wadogo, na pia kunywa damu zao katika visa vingine.