Back to top

Wanufaika wa NHIF: Mfuko ugharamie kuhifadhi miili ya wanachama wake.

20 February 2021
Share

Wanufaika wa Mfuko Wa Taifa Wa Bima Ya Afya (NHIF) wameuomba mfuko huo kufanyiwa maboresho ili kuondoa usumbufu anaoupata mwanachama pindi anapofariki kwa kuhakikisha mfuko unahudumia hadi gharama za kuhifadhi  miili ya waliokua wanachama wao ili kuepusha usumbufu ambao umekua ukijitokeza ikiwemo baadhi ya miili kung'anganiwa katika baadhi ya hospitali hapa nchini.
.
Hayo yamesemwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya wafanyakazi kutoka mikoa ya kanda ya ziwa kwenye kikao kazi cha kutoa elimu ya  mabadiliko ya sheria na kuboresha huduma za mfuko wa NHIF.