Back to top

Waokotwa baharini baada ya kukaa kwa zaidi ya siku 21.

10 June 2021
Share

Watu wawili waliojulikana kwa majina ya Hasanal mwenye umri wa miaka 39 na mdogo wake Aslahi Hasanal mwenye umri wa miaka 33 wakazi wa Anjuani nchini Comoro wamelazwa kwa dharura katika kituo cha afya cha Konde wilayani Micheweni kupatiwa huduma za awali za matibabu baada ya kuokotwa baharini ambako wanasadikiwa kukaa kwa zaidi ya siku 21.
.
Akizungumza na ITV Mkuu wa mkoa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatibu aliyefika kuwajulia hali amesema baada ya afya za watu hao kuimarika watakabidhiwa katika idara ya uhamiaji mkoani hapo kwa ajili ya utaratibu wa kuwarejesha Anjuan visiwa vya Comoro.
.
Mkuu wa idara ya uhamiaji mkoa Kaskazini Pemba amesema tayari wamewapatia huduma muhimu za kibinadamu na watawarudisha salama nchini kwao baada ya afya zao kuimarika.
.
Aidha, Daktari wa zamu aliyewapokea na kuwapatia matibabu Dk.Said Mohamed Saidi amesema hali zao zinaendelea vyema ila wapo chini ya uangalizi wa kiafya ili kuwakinga na magonjwa mengine yanayo weza kudhofisha afya zao.