
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Geita, limewalalamikia wananchi wa Mkoa huo wanaotumia muda mwingi kupiga simu ya bure ya Jeshi hilo kwa lengo la kuwasalimia Askari waliopo zamu pamoja na kuulizia uwepo wa maji ya kutosha na utayari wao, ambapo limebainisha kuwa hali hiyo inazuia wananchi wengine wenye matukio ya moto kushindwa kupata msaada.
.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Jeshi hilo, Mkoani humo, Mrakibu Hamis Dawa, ambapo amewataka wananchi wanaotaka kuwasalimia Askari wa Jeshi hilo kufika kwenye ofisi hizo, badala ya kupiga simu.