Back to top

Siku 7 zaongezwa kamati maalum mauaji Mtwara.

19 February 2022
Share

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa ameridhia kuongeza muda wa siku saba kwa kamati maalum iliyopewa jukumu la kuchunguza mauaji yaliyofanyika Mtwara na Kilindi, Tanga. 

Kamati hiyo iliyoanza kazi Februari 4, 2022 ilipaswa kukamilisha ripoti yake ndani ya siku 14, zilizoishia Februari 17, 2022.

 Kutokana na ukubwa wa kazi na mahitaji ya kujiridhisha na baadhi ya masuala, kamati imeomba kuongezewa siku saba kuanzia Februari 17 hadi Februari 23, 2022.