Back to top

WAPONA SIKOSELI BAADA YA KUPANDIKIZWA ULOTO

30 January 2024
Share

Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma, imeandika historia ya watoto watatu kupona ugonjwa wa Sikoseli baada ya kuwafanyia matibabu ya upandikizaji wa Uloto.

Hayo yamebainishwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamini Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika, wakati akitoa taarfa rasmi kwa vyombo vya habari leo Jijini Dodoma, baada ya mwaka mmoja tangu Hospitali hiyo ifanye Matibabu ya Upandikizaji wa Uloto kumtibu mtoto mwenye Ugonjwa wa Sikoseli.

Dkt.Chandika amesema watoto hao hawana maradhi ya Selimundu tena, na kwamba serikali chini ya uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, imewekeza zaidi ya Billioni 3.6 kuwezesha huduma hizo ili kuokoa maisha Watanzania.