Back to top

Wapya 147 wakutwa na corona Kenya akiwemo mtoto wa mwaka mmoja.

28 May 2020
Share

Idadi ya maambukizi ya corona nchini Kenya imefikia watu 1618 hii ni baada ya watu 147 zaidi kuthibitishwa kuwa na virusi hivyo katika muda wa saa 24 zilizopita baada ya sampuli 2831 kufanyiwa uchunguzi.

Mtoto wa mwaka mmoja wakiwa ndiye mtu wa umri mdogo zaidi miongoni mwa waliothibitishwa kuambukizwa hii leo.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe akidokeza kuwa miongoni mwa maambukizi hayo mapya 147 hao 90 ni jijini Nairobi na 41 huko Mombasa.

Vilevile idadi ya waliofariki imefikia 58 baada ya watu wengine watatu kufariki,wawili huko Mombasa na mmoja huko Kiambu.

Idadi ya waliopona imefikia 421 baada ya watu 13 zaidi kupona na kuondoka hospitalini.

Wizara ya afya ikisema kufikia sasa wahudumu wa kiafya 54 wameambukizwa virusi vya Corona hii ikiwa ni asilimia 3.5 ya maambukizi yote kwa ujumla.