Back to top

Waraibu dawa za kulevya kupewa mafunzo ya ujuzi

31 March 2022
Share

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mh.Balozi. Dkt. Pindi Chana amesema serikali inatarajia kuwajengea uwezo waraibu wa dawa za kulevya waliopata nafuu kwa kuwapatia mafunzo ya kukuza ujuzi kupitia vyuo vya ufundi katika fani mbalimbali ili kujiajiri na kuendelea kufanya shughuli za kiuchumi kuinua kipato chao na kuchangia pato la taifa.
.
Mhe. Pindi alisema Serikali kupitia Mfuko wa Dunia wa Kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund) imepata fedha kiasi cha shilingi billioni 2.4 kwa ajili ya kujenga vituo vitatu (3) vya Serikali vya kutolea huduma za utengamao kwa Waraibu wa dawa za kulevya. Vituo hivi vitajengwa katika Mikoa ya Dodoma, Dar es Salaam na Tanga.
.
“Katika mwaka wa fedha 2021/22 Serikali imeanzisha Kliniki moja ya Methadone katika Mkoa wa Arusha na ndogo nne katika Mkoa wa Dar es Salaam na kufanya jumla ya Kliniki zilizopo kuwa 15 ambazo zinatoa matibabu kwa waathirika wa dawa za kulevya nchini na Ofisi tatu za Mamlaka katika Mikoa ya Dodoma, Mtwara na Mwanza hivyo kupitia programu hii ya kukuza ujuzi wanufaika wa mafunzo hayo watapatiwa zana za kufanyia kazi”Alisema Mhe. Pindi Chana.