Back to top

Wasafiri kutoka nje ya nchi kupelekwa karantini hosteli za Magufuli .

05 April 2020
Share

Serikali imetangaza rasmi kwamba wasafiri wote kutoka nchi za nje zilizoathirika na ugonjwa wa Corona watalazimika kukaa karantini kwa muda wa siku 14 katika hosteli za Chuo Kikuu Cha Dar es  Salaam maarufu hosteli za Magufuli.

Akizungumza katika hosteli za Magufuli, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema wasafiri hao watafikia katika hosteli za Magufuli ambazo zipo katika eneo la Ubungo Jijini Dar es Salaam.

Waziri Ummy Mwalimu amewataka wananchi waelewe kwamba wasafiri hao si wagonjwa kwa sababu wanatoka kwenye nchi zenye maambukizi yenye virusi vya Corona (Covid-19) hivyo wasichukuliwe kama ni wagonjwa.

Tutawaweka hapa kwa siku 14 kwa lengo la kuwaangalia afya zao, itakapofika siku 14, wale ambao hawajaonyesha DALILI zozote tutawaruhusu waende majumbani kwao lakini wale watakaoonyesha dalili ndani ya siku tano, sita, Saba, nane hadi siku ya 14 tutachukua sampuli na kuwapima ili kujiridhisha Kama wana virusi vya Covid-19,” amesema Ummy Mwalimu.