Back to top

Washindi wa promosheni ya wakala kinara wamekabidhiwa zawadi.

09 January 2020
Share

Shindano hilo ambalo liliendeshwa na kitengo cha Tigo Pesa kwa ajili ya kutoa shukrani kwa mawakala zaidi ya 100,000 waliopo nchi nzima kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuwahudumia wateja.

Shindano hilo lilianza rasmi Desemba Mosi na ilifikia kikomo Desemba 31  mwaka jana, lilishirikisha mawakala wa Tigo Pesa nchi nzima kwa kugawanywa kwa kanda.
Kanda zilizoshiriki kwenye shindano hilo ni pamoja na Pwani, Kaskazini, Kusini na Kanda ya Ziwa.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Tigo Pesa, Angelica Pesha, alisema kuwa promosheni hiyo ilifanyika kwa ajili ya kuwashukuru mawakala wa Tigo Pesa nchi nzima kutokana na kuwahudumia wateja.

Alisema kuwa shindano lilianzia ngazi ya Kanda ambapo kila kanda walipatikana washindi wawili na baadaye wakapatikana washindi wa kitaifa.

Angelica alisema zaidi ya sh. milioni 50 zimeshindaniwa ambapo washindi wa kanda wa kwanza alipata sh. milioni tatu na wa pili alipatiwa sh. milioni mbili na jumla ya sh. milioni 20 zilishindaniwa.
 
Alisema kuwa Kampuni ya Tigo, imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanakuwa wabunifu ikiwa ni pamoja na kuandaa promosheni mbalimbali na kuwashukuru wadau wao.

Alisema anawapongeza washindi wote nchi nzima kutokana na kuibuka kidedea ambapo wanatarajia kuendesha promosheni kila wakati.

“Kama kampuni kamili ya fedha, tumekuwa tukitoa huduma mbalimbali na kwamba tunawapongeza washindi wote waliojishindia zawadi hizo na tutaendelea kuwa wabunifu kila wakati,” alisema.

Mshindi wa kwanza wa sh. milioni 20, Hajira Fadhil kutoka Ilala, alisema kuwa anaishukuru kampuni ya Tigo kutokana na kuendesha shindano hilo na kuibuka kidedea.

Alisema kuwa yeye ni mama wa watoto watano na kwamba anatarajia kutumia fedha hizo kwa ajili ya kufungua duka jingine la wakala wa Tigo Pesa ili kuhakikisha anakuza biashara yake.

Mshindi wa pili, Suleiman Hussein kutoka Zanzibar, alisema kuwa amefurahia kupata ushindi na kwamba anaimani fedha hizo zitamsaidia kuendeleza na kuboresha huduma ya uwakala.

“Nimefurahia kupata ushindi wa pili kitaifa na kwamba ninatarajia kutumia fedha hizi kuendeleza na kuiboresha biashara yangu,” alisema.