Back to top

Wasiojulikana wamuua mwalimu wa Sekondari Kigoma

10 September 2020
Share


Watu wasiojulikana wamemuua kwa kumpiga risasi mwalimu Fredrick Richard wa Shule ya Sekondari ya Kihenya katika kijiji cha Herushingo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.

Baada ya tukio hilo wauaji ambao hawakuchukua chochote katika eneo la tukio walitokomea kusikojulikana.

Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma Kamishina Msaidizi wa Polisi James Manyama amewaambia waandishi wa habari kuwa baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa ya tukio hilo, lilianza uchunguzi na kufanikiwa kumkamata mtu mmoja anayetuhumiwa kuhusika na mauaji hayo na wengine wanaendelea kutafutwa.

Aidha, amesema wakati jeshi hilo likifanya operesheni ya kuwasaka watuhumiwa wa tukio hilo, limewakamata wahamiaji haramu ishirini na mmoja wanaoishi na kufanya shughuli mbalimbali katika wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma bila kibali.