Back to top

Wastani wa chini ya asilimia 50 ya wanafunzi hawajaripoti shule Masasi

18 January 2019
Share

RC awataka wananchi kuacha kutumia suala la malipo ya korosho kama kichaka cha kutowapeleka watoto shuleni.

Wakati shule za msingi na sekondari zimefunguliwa zaidi ya wiki moja sasa, wastani wa chini ya asilimia 50 ya wanafunzi katika halmashauri ya wilaya ya Masasi na halmashauri ya mji wa Masasi mkoani Mtwara, hawajaripoti kwenye shule walizopangiwa, kwa kisingizio cha kutolipwa korosho.

Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Masasi Selemani mzee wakati akitoa taarifa juu ya maendeleo ya wilaya hiyo, kwenye kikao kilichohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali wa ngazi ya wilaya na mkoa, viongozi wa dini na wa kimila katika wilaya hiyo.

Kufuatia hali hiyo, Mkuu wa mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa amewataka wananchi kuacha kutumia suala la malipo ya korosho kama kichaka cha kutowapeleka watoto shuleni na hivyo akatoa maagizo kwa wakuu wote wa wilaya kuhakikisha wanafunzi wote wanaripoti shuleni kabla ya mwisho wa mwezi huu.