Kufuatia Viongozi wa Vyama vya upinzani, kumtaka Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Hamadi Masauni ajiuzulu, kwa madai ya kushindwa kudhibiti watu kutekwa huku wengine wakiuawa kikatili, Waziri huyo amewataka Watanzania kudumisha hali ya amani na utulivu, ili kuenzi kauli mbiu ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, ya kuleta Maridhiano, Mabadiliko, Ustahimilivu na Kujenga Upya (4R).
Waziri Masauni ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Maafisa wa Jeshi ngazi ya Taifa, Viongozi wa serikali ngazi ya Mkoa na wananchi wa Wilaya ya Lushoto alipokwenda kuzindua Jengo la Polisi la Wilaya ya Lushoto
Aidha Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani Lushoto Bw. Ally Dafa, amemwomba Mhe.Waziri Masauni kupitia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi haraka, ili wananchi wasikose imani na serikali yao.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Naibu Kamishna Narcis Misama, amesema Jeshi lake litaendelea kufanya kazi kwa weledi ili kudumisha hali ya usalama wa raia.