
Wanasarakasi wawili kutoka Tanzania maarufu kama 'Ramadhan Brothers' wameibuka washindi katika mashindano ya American Got Talent.
Wawili hao wanaoshirikisha Fadhili Ramadhan na Ibrahim Jobu, walishinda taji hilo Jumatatu usiku na kuwashinda wapinzani wao wakuu Pack Drumline, V.Unbeatable, Sainted na Musa Motha.

Kwa mujibu wa US Today, ushindi huo wa tuzo ya AGT ni safari ya miaka miwili ya vijana hao wawili.
Katika shindano hilo Ramadhani Brothers waliwashangaza waamuzi na wawashtua watazamaji kwa namna walivyocheza sarakasi hizo kwa namna tofauti.
Hatahivyo licha ya kuingia fainali kama wahitimu wakuu, walipoteza kwa mshindi wa Msimu wa 18 Adrian Stoica & Hurricane.
